Back

ⓘ Utamaduni - wa Kiafrika, wa Nigeria, Magharibi, wa Kitanzania, Kalenda ya Kichina, Mapinduzi ya utamaduni, Sherehe ya Utamaduni ya Wamaragoli, Kaburi, wa Nok ..                                               

Utamaduni wa Kiafrika

Utamaduni wa Afrika unajumuisha tamaduni zote ambazo ziliwahi kuweko katika bara la Afrika. Dhana ya utamaduni wa Afrika nzima ilijadiliwa kwa makini katika miaka ya 1960 na 1970 katika muktadha wa harakati ya Négritude, lakini imepoteza mtindo katika masomo ya Afrika. Mpasuko mkuu ni kati ya Afrika ya Kaskazini pamoja na Chad na Pembe la Afrika, ambayo ni sehemu ya ulimwengu wa Kiislamu, na Afrika ya kusini kwa Sahara, ambayo imegawanywa katika idadi kubwa ya tamaduni za kikabila, zikiwemo za Niger-Congo sanasana za Kibantu, Nilo-Saharan katika maeneo ya Sahara na Sahel na sehemu za Afrik ...

                                               

Utamaduni wa Nigeria

Utamaduni wa Nigeria umeumbwa na kabila nyingi za Nigeria. Nchi hii ina zaidi ya lugha 250 na tamaduni mbalimbali. Hata hivyo, kabila kubwa ni Hausa - Fulani ambao ndio wengi kaskazini, Igbo ambao ndio wengi kusini-mashariki na Yoruba ambao ndio wengi kusini. Makabila ya Benin yamejaa katika kanda kati Yorubaland na Niger Delta. Asilimia 80 ya Benin huwa Wakristo wakati asilimia 20 iliyobaki huwabudu Ogu. Wanafuatwa na Ibibio / Annang / Efik watu wa pwani ya kusini mashariki mwa Nigeria na Ijaw wa Niger Delta. Makabila mengine ya Nigeria wakati mwingine huitwa "mini-minorities" hupatikana ...

                                               

Magharibi

Magharibi ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande wa machweo ya jua. Magharibi ni pia jina la saa ya swala ya jioni ya Waislamu na swala yenyewe. Jina "magharibi" limetokana na neno la Kiarabu مَغْرِب maghrib linalomaanisha sehemu upande wa machweo. Magharibi kawaida huwa upande wa kushoto kwenye ramani. Tanzania iko upande wa magharibi wa Bahari Hindi, Burundi iko upande wa magharibi wa Tanzania, na nchi ya Malawi iko upande wa magharibi wa Msumbiji. Kwa maana ya kiutamaduni kuna mazoea ya kutaja utamaduni wa Ulaya pamoja na Marekani ambayo ni mtoto wa utamad ...

                                               

Utamaduni wa Kitanzania

Utamaduni ni mfumo wa maisha ya watu jinsi wanavyoishi na maendeleo yao kijamii, kiuchumi, kisiasa n.k. Tanzania ni moja kati ya nchi zinazosifika duniani kwa kulinda maadili yao. Kuna makabila yasiyopungua 120 ambayo yote hutunza mila na desturi zao kwa kiasi tofautitofauti. Mambo yanayofanya Tanzania kutunza utamaduni wake ni haya: heshima iliyopo miongoni mwa jamii hii husaidia watu kuwa na maendeleo kwa sababu ya heshima hiyo. Nyingine ni utunzaji wa watoto, wazee, vijana pamoja na walemavu ambao wote ni mazao ya jamii ambapo kila mtu katika jamii hufunzwa kuwahudumia watu waliopo kati ...

                                               

Kalenda ya Kichina

Kalenda ya Kichina ni kalenda ya kidesturi inayoitwa pia kalenda ya Han. Inatumiwa nchini China na pia na watu wanaofuata utamaduni wa kichina penginepo duniani pamoja na Kalenda ya Gregori.

                                               

Mapinduzi ya utamaduni

Mapinduzi ya utamaduni ni mageuzi ya haraka katika siasa na jamii nchini China yaliyotokea katika miaka 1966 - 1976 chini ya uongozi wa Mao Zedong, mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha China. Lengo lilikuwa kusafisha ukomunisti kutoka mabaki yoyote ya utamaduni asili wa nchi hiyo pamoja na ubepari, lakini pia kuimarisha uongozi wa Mao katika chama. Matokeo yalikuwa aina ya ibada kwa Mao, makumbusho mengi kubomolewa, dhuluma za kila namna dhidi ya mamilioni ya wananchi, watu kuhamishwa kwa lazima, nchi kupooza kisiasa pamoja na kuiathiri kiuchumi. Mapinduzi hayo yaliathiri Ulaya pia na k ...

                                               

Sherehe ya Utamaduni ya Wamaragoli

Sherehe ya Utamaduni ya Wamaragoli, ambayo hufanyikia mjini Mbale kila tarehe 26 Desemba, ni sherehe ya kutambua si tu utamaduni na turati za Wamaragoli, ila jamii yote ya Waluhya walio na makao katika Kaunti ya Vihiga. Jamii hii ya Waluhya inajumuisha Wamaragoli, Wanyore, Watiriki na majirani zao ambao ni Waidakho na Wakisa. Sherehe hii huandaliwa na Vihiga Cultural Society. Mlezi wa kwanza alikuwa Moses Mudavadi, baba wa mmoja wa mawaziri wakuu wasaidizi wawili wa nchi ya Kenya, Musalia Mudavadi.

                                               

Kaburi

Kaburi ni mahali pa kulaza maiti ya binadamu au mabaki yake. Tendo lenyewe linaitwa mazishi au maziko na mara nyingi linaendana na aina ya ibada. Linaweze kuwa na namna nyingi, kadiri ya utamaduni wa wahusika.

                                               

Utamaduni wa Nok

Utamaduni wa Nok ulikuwa ustaarabu wa kale katika maeneo ya Nigeria ya sasa. Ulitokea mnamo mwaka 1000 KK na kutoweka mnamo 300 BK. Ustaarabu huo ulitambuliwa kutokana na mabaki yake ya kiakiolojia kaskazini na katikati mwa Nigeria. Jina linatokana na kijiji cha Nok katika Jimbo la Kaduna ambako sanamu zilitambuliwa mnamo 1968 wakati wa uchimbaji katika migodi. Ufundi na ubora wa sanaa ulionyesha hali ya utamaduni wa juu, utafiti wa ardhi ambako sanamu zilikutwa ulithibitisha ni mabaki ya siku kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. Utafiti wa udongo ulionyesha pia sanamu zote zilizopatikana katika ...

                                               

Ustaarabu wa magharibi

Ustaarabu wa magharibi ni utamaduni wenye taratibu za kijamii, maadili, desturi, sheria, falsafa, imani, siasa, sanaa na teknolojia maalumu ambavyo asili yake ni Ulaya hata kame vimezidi kustawi sehemu nyingine za dunia ambazo historia yake ilikuwa na uhusiano wa pekee na bara hilo. Kwa kiasi kikubwa ni urithi wa Ugiriki wa Kale, Roma wa Kale, Uyahudi, na utamaduni wa makabila menginelakini hasa wa Ukristo na madhehebu yake ya kwanza, Kanisa Katoliki, pamoja na Makanisa ya Kiorthodoksi. Baada ya Matengenezo ya Kiprotestanti, athari yake imekuwa kubwa pia, hasa Ulaya Kaskazini na makoloni y ...

                                               

Bafu

Bafu ni chumba kilichotengwa cha kuogea ambacho walau huwa na beseni au karai la kuogea. Huenda bafu ikawa ndani ya nyumba kunakokaa watu au hata nje kando ya nyumba ile. Katika nyumba za kisasa, bafu huambatanishwa na choo. Katika jamii ya Kiamerika, neno bafu huashiria mahala pa kukogea na pia kutabawali. Kwa hivyo, mabafu yao huwa na choo ndani. Neno hili, pamoja na neno hamamu, linaweza kutaja pia jengo lenye beseni kubwa la kuogelea kwa umma wa watu wengi au watu kuoga. Kihistoria kuwepo kwa bafu au hamamu za kijamii kulikuwa taasisi muhimu kwa afya ya umma. Katika mazingira ambako te ...

                                               

Chai

Chai ni kinywaji kinachotengenezwa kwa kulowesha majani ya mchai katika maji ya moto. Wakati mwingine hata vinywaji vinavyopatikana kwa kutumia majani ya mimea mingine vinaitwa "chai". Watu hunywa chai kwa sababu inatoa uchovu. Athari hii inatokana na dawa ya kafeini iliyopo ndani ya chai sawa na kahawa.

                                               

Desturi

Desturi ni jambo lá kawaida linalotendwa na jamii fulani mara kwa mara. Neno hilo ni sawa na mazoea, ada au kaida. Kwa kawaida kila jamii huwa na desturi zake. Pia desturi huweza kutokea kwa mtu binafsi. Imezoeleka katika jamii zetu, desturi huambatana na mila. Ukichunguza kwa undani katika jamii nyingi za Afrika, mila ndiyo hujenga desturi ingawa wengi wetu tunashindwa kutofautisha dhana ya neno mila na neno desturi. Mfano wa desturi ni adabu na utaratibu wakati wa kula. Hapa utabaini kwamba, kila kabila lina mazoea yake ya kuliendea jambo hilo.

                                               

Godoro

Godoro ni kifaa kikubwa cha kusaidia mwili kupumzika. Hutumiwa kama kitanda au kama sehemu ya kitanda. Godoro huwekwa kwenye chaga ya kitanda na kulaliwa. Godoro huwa na kitambaa cha juu ambacho ndani yake huenda kukawa na sponji, nyasi, nywele au pamba. Godoro za kisasa huenda zikawa na maji au hata hewa iliyowekwa kwenye kifuko kisicho na vishimo na kitakachoweza kubeba yaliyomo ndani yake.

                                               

Itifaki

Itifaki ni orodha au mpangilio wa visa unaotumika katika kuendesha sherehe, mkutano, mjadala na kadhalika kutokana na utaratibu uliowekwa. Mathalani katika shughuli za mikutano ni kiongozi gani anatakiwa kuingia kwanza, kisha nani afuatie na nani awe wa mwisho kuingia katika sehemu ya mkutano. Mwenyeji wa mkutano anatakiwa kukaa upande gani na mgeni mwalikwa anatakiwa kukaa upande gani. Kama ni shughuli ya kitaifa ni wimbo wa taifa gani unatakiwa uanze, ule wa Rais mwenyeji au wa Rais mgeni? Baada ya mkutano nani anatakiwa kutoka kwanza na nani awe wa mwisho. Mambo kama haya au utaratibu k ...

                                               

Kanisa la kitaifa

Kanisa la kitaifa ni Kanisa la Kikristo linaloambatana na kabila au taifa fulani kiasi cha kuwa sehemu muhimu ya utamaduni wake. La kwanza lilikuwa Kanisa la Kitume la Armenia. Suala hilo lilijadiliwa hasa katika karne ya 19, wakati utaifa ulipostawi. Pamoja na hayo, aina hiyo ya Ukristo inadumu hai hasa Uingereza na Skandinavia, pengine kama dini rasmi ambayo nchi inaipa haki za pekee katika sheria zake

                                               

Kupigana

Kupigana ni kitendo cha kugombana kati ya mtu mmoja na mwingine au kikundi na kikundi au nchi na nchi n.k. Mapambano makubwa yanajulikana kama vita. Mapambano ya maneno yanajulikana kama hoja. Kupambana ni ufanisi, katika uwanja wa vita au hoja inahitaji utayari wa kupambana. Katika maeneo ya kijeshi, neno hilo linatumiwa pia kwa wafanyakazi,ambalo eneo hilo linapaswa kupokea mafunzo sahihi na kuwa na ujuzi wa kufanya shughuli za kupambana katika kitengo ambacho hutolewa. Kupigana kunaweza kufanyika chini ya sheria maalum au haijatilishwa. Mifano ya sheria ni pamoja na Mkutano wa Geneva, s ...

                                               

Mapambo ya vito

Mapambo ya vito ni vitu vya nakshi ambavyo huvaliwa katika mwili au hata katika nguo alizovaa mtu. Jina hilo hutumiwa kwa vitu vyovyote vilivyompamba mtu. Vinatumiwa hasa na wasichana, wanamitindo waliobobea katika fasheni, lakini wanaume pia huwa na mapambo yao.

                                               

Mapazia

Mapazia ni vipande vya kitambaa vilivyopangwa kuzuia mwanga, maji, vumbi n.k. lakini pia watu wasione ndani kwa sababu za faragha. Mapazia huweza pia kutumiwa kwenye kumbi za maonyesho au matukio mbalimbali kama harusi, kimapaimara na hata jukwaa la maigizo. Hutumika pia kutenganisha steji na ukumbi. Mapazia hukamilisha muonekano wa jumla wa nyumba. Mara nyingi huwekwa ndani ya madirisha ili kuzuia mwanga, kwa mfano usiku ili kusaidia usingizi. Kupima ukubwa wa pazia unaohitajika kwa kila dirisha kuna tofauti sana kulingana na aina ya pazia linalohitajika, ukubwa wa dirisha, na aina na uzi ...

                                               

Marashi

Marashi ni mchanganyiko wa mafuta na manukato yanayonukia vizuri ambayo hupulizwa au kupakwa katika mwili, nguo, viatu au hata nyumba. Marashi hufanya kunukia vizuri hata pahala palipokuwa pakinuka vibaya. Maandishi ya kale na yaliyovumbuliwa na wasomi wa akiolojia yaonyesha kwamba utumiaji wa marashi umekuwako kwa muda mrefu sana. Utumiaji wa marashi ya kisasa ulianza katika karne ya 19 baada ya kutengenezwa kwa vitu kama vanilin na coumarin.

                                               

Medali

Medali ni kipande cha metali anachopewa mshindi katika mashindano ya mchezo au mtu anayepongezwa kwa mafanikio. Watu hupewa medali kama tuzo kutokana na kufanikiwa katika jambo fulani. Thamani ya medali hutegemea na makubaliano ya tuzo husika: mtu huweza kupewa medali ya shaba, fedha, dhahabu n.k.

                                               

Michezo

Michezo ni amali au mazoezi ya kimwili ambayo mara nyingi yana ushindani ndani yake. Yanatendeka kufuatana na kawaida na taratibu maalumu zilizokubaliwa kati ya wachezaji au katika jamii. Michezo ni ya aina nyingi ikiwemo michezo ya juu angani, majini, kwenye nchi kavu na pia kwenye barafu. Watu hushiriki kwenye michezo kushindania zawadi, kama aina ya mazoezi au kujiburudisha tu. Kuna michezo ambayo huhusisha mwili kama vile mbio ambazo huwa na vitengo tofautitofauti, miereka, dodi, kareti, judo, taekwondo, kuruka juu, kuruka urefu, kuogelea n.k. Kuna michezo inayohusisha akili kama vile ...

                                               

Michezo ya watoto

Michezo ya watoto ni michezo mbalimbali inayochezwa na watoto. Mara nyingi michezo hiyo huigiza maisha halisi ya jamii. Watoto hucheza kutokana na tamaduni zao, kwa mfano kama utamaduni wa eneo hilo ni ngoma basi mara nyingi watoto watacheza na kupiga ngoma licha ya kuchanganya na michezo mingine. Michezo ya watoto huwasaidia kukua kiakili na kimwili pia. Ni muhimu watoto waweze kushiriki michezo mbalimbali kwa madhumuni ya kuwajenga. Michezo ya watoto ipo ya aina mbalimbali, kwa mfano Afrika Mashariki kuna: Kombolela butuo Ulingo bayoyo Buye Bembea Kukimbia na kijiko Kuruka Kibereko Mdako ...

                                               

Miwani

Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama hapa Miwani ni kifaa cha msaada wa kuona vizuri zaidi kinachotumiwa na watu wenye macho mabovu. Ni kifaa kinachoboresha uwezo wa kuona. Kwa kawaida miwani ni lenzi mbili za kioo au plastiki zinazoshikwa na fremu. Fremu hulala juu ya pua ikiwa na mikono miwili inayoshikana na masikio. Aina za lenzi zinateuliwa kutokana na udhaifu wa macho yaani tabia ya lenzi inapaswa kulingana na tatizo la kila jicho. Kuna pia miwani ya kukinga macho ama dhidi ya jua kali au dhidi ya upepo na vumbi wakati wa kufanya kazi au kwenye burudani ya michezo. Kundi la madak ...

                                               

Muziki

Muziki ni aina ya sanaa inayotumia sauti mbalimbali: za kibinadamu na za ala za muziki, ama kwa pamoja au kila moja pekee. Asili ya neno iko katika lugha ya Kigiriki ambamo huitwa μουσική mousikee. Baadhi ya sifa za muziki ni uzito wa sauti pitch na wizani au mahadhi rhythm. Aina ya muziki inayopatikana kote duniani ni nyimbo ambazo ni maneno yanayotolewa kwa sauti na mahadhi fulani mara nyingi pamoja na ala za muziki. Kwa wanaorekodi sauti, wao huenda kwa studio kurekodi na huchukuliwa kwa kinasasauti kilichoambatanishwa na tarakilishi na kudhibitiwa na kompresa.

                                               

Ngao

Ngao ni silaha ya kujihami ambayo ilikuwa inatumiwa na jamii mbalimbali za Afrika, kama vile Wangoni, Wazulu, Waxhosa na wengineo hata katika mabara mengine. Ngao zimejengwa tofautitofauti kwa nyakati tofauti pia, hata ngozi za wanyama zilitumiwa, na ukubwa na uzito ulikuwa tofauti pia. Ngao bado hutumiwa na vikosi vya polisi na jeshi leo. Ngao nyingi sasa hutengenezwa kwa vifaa vya juu, pamoja na elektroniki. Ngao zinatofautiana na si tu ngao za mkononi, lakini pia nguo, kama vile fulana, glavu na buti. Pia ngao huonekana kwenye nembo za taifa kama utambulisho kwa nchi nyingine, kwa mfano ...

                                               

Nguo

Nguo ni kitambaa ambacho kinaweza kutumika kufunikia meza, kitanda n.k. lakini hasa kutengenezea mavazi mbalimbali yanayovaliwa na mtu kwa ajili ya kujisitiri, kwa sababu ya kutunza heshima yake na kujikinga dhidi ya baridi, jua, mvua n.k. Ndiyo sababu mara nyingi neno "nguo" linamaanisha mavazi yenyewe. Nguo huvaliwa kulingana na hali ya hewa na mazingira fulani, lakini pia kulingana na mitindo inayobadilikabadilika kadiri ya nyakati.

                                               

Njemba

Njemba ni viumbe vikubwa vyenye nguvu za ajabu na ukubwa wa mwili. Katika hadithi mbalimbali, neno njemba limeundwa mwaka wa 1297. Katika hadithi nyingi za Ulaya, njemba hujulikana kama viumbe vya kwanza ambavyo vinahusishwa na machafuko, na mara nyingi hupambana na miungu. Njemba hawa huwa na hasira kali pale wanapoona miungu mbalimbali. Baadhi ya manjemba huitwa Nephilim, neno ambalo mara nyingi hutafsiriwa kama njemba ingawa tafsiri hii haikubaliki ulimwenguni. Wao ni pamoja na Og, Mfalme wa Bashani, Wanefili, Anaki, na majeshi ya Misri yaliyotajwa katika Mambo ya Nyakati 1:11:23. Kutem ...

                                               

Nyimbo za jadi

Nyimbo za jadi ni nyimbo zinazoimbwa na watu wa kabila fulani kama sehemu ya utamaduni wao. Jamii huimba nyimbo hizo kama sehemu ya utamaduni wao lakini pia huwaburudisha kutokana na staili zao za uchezaji na hata uimbaji pia. Nyimbo za asili zina umuhimu mkubwa katika maisha kwani humfanya mtu afurahie kwa kuwa katika kabila lenye nyimbo nzuri na za kuvutia. Kwa mfano Tanzania kuna makabila yanayoadhimisha na kuimba nyimbo hizo: Wamakonde huimba sindimba, Wapogoro huimba sangura n.k. Makabila mbalimbali huimba nyimbo hizo kwa lengo la kuburudika, kufurahia jambo n.k.

                                               

Osh Uzbek Music na Drama Theater

Kipala 17:25, 16 Septemba 2018 Osh Uzbek Music na Drama Theater ni uwanja wa kale wa wataalamu huko Kyrgyzstan, uwanja wa pili wa ukumbi wa michezo huko Asia ya Kati.

                                               

Sanaa

Sanaa ni ufundi anaoutumia mwanadamu ili kuwasilisha fikra au mawazo yaliyo ndani ya akili yake. Vilevile sanaa ni uzuri unaojiibua katika umbo lililosanifiwa. Kusanifu ni kuumba, kufanya jambo au kitu kwa kutumia ufundi/ustadi ili kiweze kuvutia watu kwa uzuri wake. Mtu hueleza hisia zinazomgusa kwa kutumia umbo fulani ambalo limesanifiwa. Hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemewa ioneshe ufundi wa hali ya juu ili iwe na mvuto kwa hadhira yake. Tunaweza kuona kazi ya sanaa kupitia tanzu za fasihi, uchoraji, ususi, ufumaji, utarizi, uchongaji, ufinyanzi na kadhalika. Kila umbo huwa na nyenzo ...

                                               

Taasisi ya Goethe

Taasisi ya Goethe ni taasisi ya kiutamaduni yenye shabaha ya kufundisha lugha ya Kijerumani na kujenga mawasiliano ya kiutamaduni kote duniani.

                                               

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ni taasisi ya kiserikali ya mafunzo, utafiti na ushauri katika sanaa. Taasisi hiyo ilianzishwa rasmi na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa na lengo la kutoa elimu ya sanaa, kutangaza sanaa na utamaduni, kutoa elimu ya kimaadili kwa wasanii, elimu ya filamu na elimu nyingine kwa faida ya jamii na wasanii.

                                               

Tatuu

Tatuu ni aina ya mchoro katika mwili ambao hufanywa kwa kuingiza wino na rangi kwenye safu ya ngozi. Inaweza kuwa ya kudumu au ya muda mfupi. Tatuu huanguka katika makundi matatu mapana: mapambo tu bila maana maalumu; mfano kwa maana maalumu inayomhusu aliyechorwa; picha mfano wa mtu maalumu au kipengee.

                                               

Uchale

Uchale ni undugu unaofanywa kati ya watu wawili ambao hawana undugu wa kuzaliwa kwa kuchanjiana damu. Mviga wa uchale na sababu zake hutofautiana kulingana na mila na tamaduni za watu wanaofanya undugu namna hiyo. Leo, uchale hufanyika katika magenge na baadhi ya vikundi vya uhamasishaji. Kuchanjiana damu kunaweza kueneza maradhi.

                                               

Unyago

Unyago ni mchakato wa kuingiza mtu katika hatua mpya ya maisha yake ndani ya jamii kwa jumla au jamii maalumu. Bila kupitia unyago mtu anatazamwa kama hayuko tayari kupokea majukumu mapya. Mara nyingi mchakato huo unategemea dini au utamaduni fulani, lakini unapatikana kwa namna moja au nyingine katika makundi yote ya binadamu, kutokana na mangamuzi kwamba mtu hawezi kufanya ghafla mambo mapya kabisa kwake bila kupata msaada wowote. Anthropolojia inaonyesha kwamba unyago ulikuwepo tayari katika historia ya awali. Umuhimu wa pekee ulitiwa katika mtoto kuelekea majukumu ya utu uzima kama mum ...

                                               

Usanii

Usanii ni neno lenye maana pana sana. Kwa kifupi ni ubunifu wa vitu mbalimbali unaofanana na uumbaji. Mtu anayejishughulisha na usanii huitwa msanii, na kile alichokibuni au kukiumba huitwa sanaa. Wasanii wengi wanaamini kuwa Mungu ni msanii mkubwa wa kwanza, kwa sababu ndiye aliyeumba vitu vyote, ambavyo wasanii, hasa wa uchoraji, huviiga na kuvibadili kidogo. Hapa ndipo ubunifu unapochukua nafasi katika usanii. Msanii kupitia vitu anavyoviumba, kama ni picha ya kuchora au muziki, hapo hupata nafasi ya kueleza hisia zake za ndani, k.mf. furaha, au ya wengine, huzuni yake au ya wengine, ku ...

                                               

Usimilishaji

Usimilishaji ni jinsi watu kutoka utamaduni au kabila dogo hufanywa kuwa na mila na kuzichukua tamaduni za kabila kubwa au inayotawala. Watu waliosimilishwa kikamilifu hukosa sifa za kuwatofautisha ila tu kimwili. Usimilishaji unaweza kufanyika kwa kutumia nguvu au kutumia mambo ya kitamaduni, k.v. ndoa za kabila tofauti. Hata hivyo mara nyingine mchakato huo unatokana na hiari ya watu wanaopenda utamaduni wa kigeni na kuuiga hata kupotewa na utambulisho wao.

                                               

Utani

Utani ni maneno ya mzaha yenye ukweli ndani yake. Utani kama kipengele kimojawapo cha sanaa na maigizo huonesha uhusiano mwema wa jamii unaowawezesha wanajamii hao kufanyiana maneno ya mzaha na hata kuchukuliana vitu bila kukasirikiana. Utani unaweza kuwa kati ya mtu na mtu, ukoo na ukoo au kabila na kabila. Katika nchi ya Tanzania umechangia sana kumaliza au kuepusha vita na shari nyingi baada ya makabila adui kuamua kutambuana kama watani, k.mf. Wangoni na Wahehe. Umuhimu wa utani Kuimarisha upendo, umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wanajamii kujenga undugu. Mtani ndiye mtend ...

                                               

Vuvuzela

Vuvuzela, wakati mwingine inaitwa "lepatata" au pembe la uwanjani, ni kipuliza pembe, takriban mita moja kwa urefu, barugumu hii kwa kawaida hutumika na mashabiki haswa wa mipira wa kandanda nchini Afrika Kusini. Asili ya jina haijulikani. Inaweza kuanzisha kutoka kwa waZulu kwa ajili ya "kufanya kelele," kutoka kwa sauti ya"vuvu" au kutoka mjini misimu kuhusiana na neno "oga." mbelini iliundwa nje na bati, vuvuzela ilikua maarufu katika Afrika Kusini katika miaka ya 1990. Mwaka wa 2001, kampuni yenye makao Afrika Kusini Masincedane Sport ilianzisha molekuli-mazao iina ya plastiki huhitaji ...

                                               

Zulia

Zulia ni aina ya kitambaa kinene ambacho mara nyingi hutumiwa kufunika sakafu. Mazulia hutumiwa kwa madhumuni mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhami miguu ya mtu kutoka kwenye ubaridi wa sakafu ya saruji, kufanya chumba kuwa kizuri zaidi kama mahali pa kukaa sakafu kwa mfano, wakati wa kucheza na watoto au kama mahali pa sala, kupunguza sauti ya kutembea hasa katika majengo ya ghorofa na kuongeza mapambo au rangi kwenye chumba. Mazulia hutengenezwa kwa rangi yoyote kwa kutumia nyuzi tofauti za rangi. Kuanzia miaka ya 2000, mazulia yanatumiwa pia katika viwanda, maduka ya rejareja na hoteli. ...

Orodha ya Urithi wa Dunia katika Afrika
                                               

Orodha ya Urithi wa Dunia katika Afrika

1986 - Utamaduni - Zimbabwe Kuu 2003 - Utamaduni - Hifadhi ya Taifa ya Matobo 1984 - Asili - Hifadhi ya Taifa ya Mana Pools 1986 - Utamaduni - Khami

Wizara ya Utamaduni na Utalii (Uturuki)
                                               

Wizara ya Utamaduni na Utalii (Uturuki)

Wizara ya Utamaduni na Utalii ni ofisi ya wizara ya serikali ya Jamhuri ya Uturuki, inahusika na masuala ya utamaduni na utalii nchini Uturuki. Kwa mwaka wa 2018, inaongozwa na Mehmet Ersoy.

Ukoo
                                               

Ukoo

Ukoo ni chanzo na muunganiko wa familia kadhaa zenye asili moja. Mara nyingi huwa na utamaduni na lugha moja. Ukoo huundwa na vizazi mbalimbali ambapo mila na desturi zao huendelezwa na kuhifadhiwa kwa faida ya vizazi vya baadae. Mfano mmojawapo ni ukoo wa Mkwawa uitwao ukoo wa Mwamuyinga.

Ahadi
                                               

Ahadi

Ahadi ni hali ya kuaminisha au kumuaminishia mtu au watu juu ya jambo fulani ambalo unatarajia kulitimiza na kulitekeleza kwa mtu au watu. Kwa mfano, ahadi yaweza kutolewa kama zawadi, shukrani na hata pongezi kwa mtu fulani. Msemo muhimu unafundisha kwamba "Ahadi ni deni". Hata hivyo mara nyingi ahadi ni za uongo au hazitimizwi kwa wakati uliopangwa.

Doria
                                               

Doria

Doria ni kundi la wafanyakazi, kama vile maafisa wa utekelezaji wa sheria au wafanyakazi wa kijeshi, ambao ni wa kufuatilia eneo fulani la kijiografia kuwa ni salama. Watu ambao wanafanya doria hulipwa kiasi fulani cha fedha, pia hutumia silaha mbalimbali kama bunduki, kirungu cha mpingo n.k.

Fimbo
                                               

Fimbo

Fimbo ni kijiti kirefu ambacho kinatumika kwa namna nyingi ili kufikia mbali kuliko mkono wa mtu. Kwa mfano fimbo hutumika kuua nyoka au kutoa adhabu kwa kuchapa mtoto kutokana na kosa fulani. Katika michezo mbalimbali, kama kriketi, baseball, mchezo wa pool na mingineyo.

                                               

Tuesday Kihangala

Tuesday Kihangala ni mwongozaji na mtunzi wa filamu kutoka nchini Tanzania. Aliwahi kuigiza kidogo sana katika kundi la sanaa la Kaole, na baadaye kwenda kujianzishia kundi lake mwenyewe la maigizo ya sanaa nchini Tanzania. Kundi linakwenda kwa jina la "Fukuto" lenye makazi yake huko Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tanzania. Hivi karibuni wanatamba na tamthilia ya Jumba la Dhahabu, inayoonyeshwa na Televisheni ya Taifa ya Tanzania.

                                               

Kikuba

Kikuba ni pambo la manukato linalotengenezwa kwa kulichaganya pamoja na asumini, rehani, kilua na mkadi ambalo huvaliwa shingoni au huwekwa juu ya matiti ya mwanamke kumpendezesha na huwa na harufu nzuri.

Leso
                                               

Leso

Leso ni kitambaa cha kawaida chenye umbo la mraba kilichotengenezwa kwa pamba au nguo nyingine ambayo inaweza kuingia katika mfuko au mkoba, na ambayo ina lengo la usafi wa binafsi kama kuifutia mikono au uso, au kufutia damu, lakini hasa kamasi.

Poppet
                                               

Poppet

Poppet ni midoli ambayo hufanywa kama kuwakilisha mtu, lengo likiwa kusaidia kwa mambo ya kichawi. Mara kwa mara hupatikana ndani ya moshi. Wanasesere hawa wanaweza kutengenezwa kutokana na vifaa kama vile mzizi wa kuchonga, nafaka au miti ya mahindi, matunda, karatasi, nta, viazi, udongo, matawi, au kitambaa kilichosheheni mimea kwa nia ya kuwa vitendo vyovyote vimefanya sanamu itahamishiwa kwa somo kulingana na uchawi wa huruma.

Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →