Back

ⓘ Historia - Historia, ya awali, ya Afrika, ya Uturuki, ya Uhindi, ya Lithuania, ya Moroko, ya Denmark, ya Kirgizia, ya Eswatini, Lango: Historia, Akiolojia ..                                               

Historia

Historia ni somo kuhusu maisha ya binadamu na utamaduni wao wakati uliopita. Mara nyingi neno hilo lina pia maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu kwa mfano "historia ya ulimwengu". Historia ni hasa mfululizo wa habari za mambo yaliyotokea pamoja na sababu zake. Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani. Historia inatufundisha kuishi: kumbukumbu za mambo ya zamani zinatuwezesha kuendelea vizuri zaidi. Wanahistoria wanapata maarifa yao kutoka maandishi ya zamani hasa kwa historia andishi ...

                                               

Historia ya awali

Historia ya awali ni kipindi kirefu sana cha historia, kikichukua miaka yote tangu binadamu walipotokea duniani mpaka historia andishi ilipoanza. Ingawa muda ni mrefu sana na ni wa msingi kwa historia yote iliyofuata, watu hawakuwa wengi kama walivyozidi kuwa kadiri ya maendeleo yao. Maisha yao hayakuwa marefu kutokana na ugumu wa mazingira na utovu wa vifaa na dawa mbalimbali.

                                               

Historia ya Afrika

Historia ya Afrika ni historia ya bara hilo lililo asili ya binadamu wote. Kwa ujumla, historia ni kumbukumbu ya maisha ya mwanadamu duniani, hasa ile tarehe iliyosajiliwa na kuhifadhiwa katika vitabu, maandishi mbalimbali, na simulizi au hekaya za mapokeo. Ingawa historia iliyobebwa katika simulizi na hekaya huchukuliwa na baadhi kuwa haina nguvu kwa kukosa ithbati ya maandishi, bado hivi ni vyanzo muhimu vya historia. Mara nyingi historia iliyoko katika maandishi huwa imehifadhiwa katika simulizi na hekaya kwa muda mrefu kabla ya kuandikwa.

                                               

Historia ya Uturuki

Waturuki waliwahi kuwa kiini cha Milki ya Osmani pia: Ottomani iliyounganisha mataifa mengi chini ya Sultani wa Konstantinopoli. Hilo dola kubwa lilitawala upande wa mashariki wa Mediteranea pamoja na nchi nyingi za Mashariki ya kati ya karne ya 14 na mwaka 1922. Milki ilianzishwa na Waturuki Waosmani ikachukua nafasi ya ukhalifa wa Waabbasi na Milki ya Bizanti. Mji wake mkuu ulikuwa Konstantinopoli leo: Istanbul na mtawala wake mkuu alikuwa Sultani wa Waosmani. Imani rasmi ya milki ilikuwa Uislamu hata kama katika maeneo mengi idadi kubwa ya wakazi walikuwa Wakristo. Tabaka la viongozi wa ...

                                               

Historia ya Uhindi

Binadamu walifika India kutoka Afrika kabla ya miaka 55.000 iliyopita. Uwepo wao wa muda mrefu, kwanza kama wawindaji-wakusanyaji waliozagaa barani, umefanya watu wa eneo hilo wawe na tofauti kubwa kati yao upande wa urithi wa kibiolojia, ambayo inapitwa na Waafrika tu. Makazi ya kudumu yalianza magharibi, katika beseni la mto Indus, miaka 9.000 iliyopita, hata kuzaa ustaarabu maalumu Indus Valley Civilisation katika milenia ya 3 KK.

                                               

Historia ya Lithuania

Kuanzia karne ya 13 Lithuania ilikuwa nchi huru na imara iliyoteka maeneo mengi; kufikia karne ya 15, ikiwa pamoja na Polandi, ilikuwa kubwa kuliko nchi zote za Ulaya. Mwaka 1795 nchi hizo mbili zilifutwa, na Lithuania ikawa sehemu ya Dola la Urusi. Mwaka 1918, ikawa tena nchi huru, lakini mwaka 1940 Warusi waliiteka tena. Miaka 1940 - 1990 nchi ilikuwa jamhuri mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti. Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Lithuania ilijitangaza nchi huru. Lithuania imekuwa nchi mwanachama ya Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.

                                               

Historia ya Moroko

Habari za kimaandishi za kwanza ni kutoka karne za kwanza KK. Wafinisia walijenga miji yao pwani lakini eneo la ndani lilibaki nchi ya Waberber waliounda ufalme wa Mauretania ya Kale usiuchanganye na nchi ya kisasa Mauretania uliounganisha sehemu kubwa ya Moroko ya kaskazini. Wamauretania wa kale walishirikiana na Dola la Roma hadi kuwa jimbo la dola hili kwa jina la "Mauretania Tingitana". Wakati wa kudhoofika kwa Dola la Roma kuanzia mwaka 400 BK kukawa na uvamizi wa Wavandali.

                                               

Historia ya Denmark

Utafiti wa akiolojia umeonyesha ya kwamba Denmark iliwahi kuwa na vikundi vya wawindaji tangu muda mrefu sana. Lakini katika nyakati za kupanuka kwa barafuto za Skandinavia walipaswa kundoka tena. Eneo la Denmark lilifunikwa kabisa na barafu hadi takriban miaka 13.000 hadi 15.000 iliyopita. Tangu mwaka 4000 K wakulima walianza kupatikana nchini. Hakuna uhakika kama Denmark ilikaliwa na Wakelti; kuna mabaki ya kiakolojia ya kuonyesha athira ya Kikelti, lakini haijulikani kama ni kutokana na biashara na maeneo ya Wakelti walioendelea zaidi au kama Wakelti wenyewe walikaa hapa.

                                               

Historia ya Kirgizia

Historia ya Kirgizia inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Kirgizia. Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikirgizi". Ilipata uhuru wake katika mwendo wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti. Kabla ya uhuru yalitokea mabadiliko katika uongozi wa chama cha kikomunisti. Viongozi wapya waliotafuta njia bila udikteta mkali walishika uongozi na rais Askar Akayev alirudishwa madarakani katika uchaguzi wa kwanza na wa pili. Lakini uchaguzi wa mwaka 2005 ulionekana haukuwa huru, hivyo hasira ya wananchi ikalipuka katika m ...

                                               

Historia ya Eswatini

Historia ya Eswatini inahusu eneo la Kusini mwa Afrika ambalo wakazi wake leo wanaunda Ufalme wa Eswatini. Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani. Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Waswati walianzisha ufalme wao katikati ya karne ya 18 chini ya Ngwane III; mipaka ya sasa ilikubalika mwaka 1881. Baada ya vita kati ya Waingereza na Makaburu, Swaziland ilukuwa nchi lindwa ya Uingereza tangu mwaka 1903 hadi 1967. Chini ya mfalme Sobhuza II aliyetawala kwa muda mrefu sana 1921-1982, Swaziland ilipata uhuru tarehe 6 Septem ...

                                               

Lango: Historia

                                               

Akiolojia

Akiolojia ni somo linalohusu mabaki ya tamaduni za watu wa nyakati zilizopita. Wanaakiolojia wanatafuta vitu vilivyobaki, kwa mfano kwa kuchimba ardhi na kutafuta mabaki ya majengo, makaburi, silaha, vifaa, vyombo na mifupa ya watu.

                                               

Anno Domini

Anno Domini ni namna ya kutaja miaka katika kalenda ama Kalenda ya Gregori au Kalenda ya Juliasi. Jina kamili ni "Anno Domini Nostri Jesu Christi" Mwaka wa Bwana wetu Yesu Kristo likirejea idadi ya miaka tangu kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Katika lugha ya Kiingereza ni njia ya kawaida ya kutaja miaka kama "AD" ambayo ni sawa na matumizi ya BK au "BC" yaani "before Christ" tazama KK; ni pia kawaida katika maandiko ya kihistoria yanayotumia lugha ya Kilatini.

                                               

Anthropolojia

Anthropolojia ni fani ya elimu inayochunguza pande zote binadamu kuanzia wale wa kale. Matawi yake mbalimbali yanachunguza maisha ya jamii, utamaduni pamoja na taratibu na tunu, athari ya lugha, mabadiliko ya kimwili n.k. Kwa vyovyote, anthropolojia inahitaji ushirikiano wa sayansi mbalimbali, ikiwemo teolojia. Akiolojia inaweza kutazamwa kama sehemu ya anthropolojia k.mf. Marekani au ya historia, lakini pia kama fani ya pekee k.mf. Ulaya.

                                               

Baada ya Kristo

Baada ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo ni namna ya kutaja miaka ambayo imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani. Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake Yesu huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifupi: KK.

                                               

Chimbuko la mwanadamu

Chimbuko la mwanadamu ni suala linalochochea utafiti mwingi wa akiolojia, ili kuelewa wapi walitokea watu wa kwanza. \ Suala hilo ni muhimu kwa fani mbalimbali, dini ikiwemo. Kwa sasa wataalamu karibu wote wanakubaliana kwamba chimbuko la mwanadamu lilikuwa barani Afrika, lakini wanaleta ushahidi tofauti ili kupendekeza Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika, Afrika Magharibi au Afrika Kaskazini. Sehemu ya bonde la Ufa lijulikanalo kama bonde la Oltupai lililoko ndani ya Hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania ndiko kulikogunduliwa masalia ya kale kuliko yote yanayojulikana hivi sasa kati ya viu ...

                                               

Eneo la kudhaminiwa

Eneo la kudhaminiwa lilikuwa eneo lililokabidhiwa na umma wa kimataifa mikononi mwa nchi iliyotakiwa kulisimamia. Katika karne ya 20 maeneo ya kudhaminiwa yalikuwa aina ya pekee ya ukoloni. Utawala wa mkoloni ulitekelezwa rasmi kwa niaba ya nchi huru zote za Dunia. Hali hii ya pekee ilikuwa na umuhimu hasa wakati wa uhuru wa nchi hizo. Maeneo hayo yalianzishwa mwaka 1919 katika Mkataba wa Versailles uliounda Shirikisho la Mataifa lililokuwa mtangulizi wa Umoja wa Mataifa wa leo. Nchi tawala za maeneo ya kuadhiminiwa zilipokea maeneo yale chini ya masharti ya katiba ya Shirikisho la Mataifa ...

                                               

Historia ya Ghana

Kuna ushahidi kutoka kwa maarifa ya mambo ya kale ambao unaonyesha kwamba watu wameishi katika eneo linalojulikana siku hizi kama Ghana kutoka karibu miaka ya 1500 KK Kabla ya Kristo. Licha ya hayo, hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa wakazi hao wana uhusiano na wale wa eneo hili kwa sasa. Kwa mujibu wa mapokeo simulizi, mengi kati ya makabila ya Ghana, leo kama vile watu wa chimbuko la makabila kadhaa kama Waakan, Waga na Waewe, walifika Ghana mnamo karne ya 13. Mengi ya maeneo ya Ghana yanajumuisha eneo lililokuwa la Himaya ya Ashanti, mojawapo ya falme zilizokuwa na ushawishi mkubwa katik ...

                                               

Historia andishi

Historia andishi ni kipindi cha historia ya binadamu kuanzia walipobuni uandishi miaka 3.300 hivi KK huko Mesopotamia. Hatua hiyo imewezesha kutunza kumbukumbu kwa makusudi na hivyo kuchangia sana maendeleo ya fani ya historia.

                                               

Historia na Maendeleo ya Mji wa Dar es Salaam

Dar es Salaam ilikuwa ikiitwa" Mzizima”, ni mji wa zamani ulioanza mwanzoni mwa miaka ya 1857. Ingawa historia ya Mzizima ilianza tangu miaka 1000 iliyopita ambapo watu wa Barawa ambao walitulia na kulima katika maeneo ya mbwa maji magogoni, Mjimwema na Gezaulole. Mji ulianza kuonesha mabadiliko kutokana na ujio wa Masultani, Wajerumani na Waingereza. Mwaka 1866 Sultan Seyyed Majid of Zanzibar aliupa jina la ambalo ndilo linalotumika sasa neno la kiarabu lililomaanisha" Mbingu ya Amani”. Baaba ya kifo cha Sultan Majid mwaka 1870, Dar es Salaam ilianguka lakini iliinuka tena mara baada ya u ...

                                               

Historia ya Asia

Historia ya Asia inaonekana kama historia ya pamoja ya maeneo kadhaa tofauti kama vile: Asia ya Mashariki, Asia ya Kusini na Mashariki ya Kati. Kwa jumla maeneo ya pembeni ya Asia, yaani Mesopotamia, India, na Uchina, yaliyozunguka mabonde yenye maji na rutuba, kwa sababu udongo wa hapo ulikuwa na uwezo wa kuzaa mazao mengi, yalikuwa asili ya maendeleo na baadhi ya dini za mwanzo kabisa ulimwenguni. Kila moja ya maeneo hayo matatu yaliendeleza ustaarabu kwa kuendeleza maendeleo ya zamani, huko likishirikiana na kufanana na mengine mawili kwa namna nyingi na kwa kufaidika na uwezekano wa ku ...

                                               

Historia ya biolojia

Historia ya biolojia inapitia maendeleo ya somo hilo muhimu la sayansi. Ingawa biolojia katika mtindo wake wa kisasa ni hatua ya hivi karibuni, sayansi zinazohusiana na zinazojumuishwa ndani yake zimechunguzwa tangu kale. Falsafa ya maumbile ilisomwa tangu siku za ustaarabu wa kale wa Mesopotamia, Misri, Bara Hindi na China. Hata hivyo, asili ya biolojia ya kisasa na mtazamo wake kwa utafiti wa viumbe mara nyingi hupata asili yake kwa Ugiriki wa kale. Huku mafunzo rasmi ya udaktari yakiwa yalianza wakati wa Hippokrates 460 KK hivi - 370 KK hivi, ni Aristotle 384 KK - 322 KK ambaye alichang ...

                                               

Historia ya Intaneti

Intaneti ni mfumo mkubwa ambao mamilioni ya kompyuta na mifumo na uendeshaji wa mfumo wa aina zote yanaweza kuwaunganisha. Hii ina maana ya mahusiano ya dunia yote pamoja. Historia yake inaweza kuanza na uzinduzi wa Sputnik na USSR uliochochea Marekani kuanzisha shirika la utafiti wa juu wa miradi, iliyojulikana kama ARPA, katika mwezi Februari 1958 ili kuongoza kiteknolojia. ARPA ilitengeneza ofisi ya teknolojia za kuchambua habari IPTO ili kuendeleza utafiti wa programu inayojitekeleza ya mazingira ya chini Sage, ambayo iliunganisha mifumo ya rada za nchi nzima kwa mara ya kwanza. J. C. ...

                                               

Historia ya maeneo ya Pasifiki

Historia ya Maeneo ya Pasifiki inahusu historia ya watu kwenye visiwa vya Pasifiki. Historia hiyo huangaliwa kufuatana na kanda zake kama vile Polinesia, Melanesia na Mikronesia; mara nyingi historia inaangaliwa pamoja na Australia na Nyuzilandi.

                                               

Historia ya tarakilishi

Historia ya tarakilishi inasimulia hatua za maendeleo ya tarakilishi toka aina ya kizamani hadi aina ya kisasa zaidi. Hatua hizo zinachukuliwa kama vizazi vya Tarakilishi. Kimsingi tarakilishi ni kifaa chochote kinachomsaidia binadamu kufanya hesabu. Zipo tarakilishi za aina mbili: za kianalojia za umakanika na za kidijiti za elektroniki. Za kwanza hazitumii umeme, na ndizo ambazo zilianza kabla ya tarakilishi za kidijiti zinazotumia umeme.

                                               

Historia ya Ufalme wa Muungano

Historia ya Ufalme wa Muungano inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Ufalme wa Muungano. Milki kubwa kwenye kisiwa cha Britania ilikuwa Uingereza. Tangu mwaka 1284 Welisi ilitawaliwa na Uingereza na katika Hati ya Muungano Act of Union ya mwaka 1536 ilikuwa sehemu ya Milki ya Uingereza. Hati ya Muungano ya mwaka 1707 iliunganisha milki mbili za Uingereza na Uskoti kuwa Milki ya Britania Kuu. Nchi zote mbili zilikuwa chini ya mfalme mmoja tangu mwaka 1603. Tangu wakati uleule Ufalme wa Eire Ireland ilitawaliwa na Uingereza pia. Sheria ya mwaka 1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Uf ...

                                               

Homo

Homo ni jenasi ambayo katika uainishaji wa kisayansi inajumlisha binadamu na spishi zilizokoma zilizofanana naye sana. Wanasayansi wamependekeza zaidi ya spishi 12 za jenasi Homo. Jina Homo ni la Kilatini, likiwa na maana ya "mtu", na kwa asili linahusiana na neno humus, "ardhi".

                                               

Koloni nyakati za kale

Makala hii inaangalia matumizi ya neno "koloni" katika mazingira ya Mediteranea katika nyakati za kale Koloni zilikuwa njia ya kueneza utawala wa nchi au taifa tangu enzi ya Wagiriki na Waroma wa kale.

                                               

Maajabu ya dunia

Maajabu ya dunia ni orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana na Wagiriki wa Kale. Wagiriki waliita majengo hayo ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ ta hepta theamata tes oikumenes - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa). Mara ya kwanza majengo ya ajabu yaliorodheshwa na mwandishi Herodoti mnamo 450 KK. Ilhali maandiko yake hayakuhifadhiwa, habari hii inatokana na waandishi wengine waliomrejea. Kulikuwa na orodha tofauti lakini ile inayojulikana na kutajwa zaidi ni ile ya Antipater wa Sidon Ilhali orodha hii ilikusanywa na waandishi wa Ugiriki ya Kale kuna majengo tu yaliyojulikana katika usta ...

                                               

Mapinduzi ya Viwandani

Mapinduzi ya Viwandani yalikuwa kipindi kutoka karne ya 18 hadi karne ya 19 ambapo yalitokea mabadiliko makubwa katika kilimo, utengenezaji wa bidhaa, uchimbaji wa madini na uchukuzi yakiwa na matokeo makubwa kwa hali ya kiuchumi, ya kijamii na ya kitamaduni. Yalianzia Uingereza na hatimaye kuenea Ulaya nzima, Amerika ya Kaskazini na mwishowe duniani kote. Mwanzo wa Mapinduzi ya viwanda ulidokeza mabadiliko muhimu katika historia ya binadamu; karibu kila kipengele cha maisha ya kila siku hatimaye yaliathirika kwa njia fulani. Mwanzo wa wakati wa mwisho wa karne ya 18 mabadiliko katika baad ...

                                               

Masijala ya Taifa (Brazil)

Masijala ya Taifa ya Brazil ni kiungo cha mfumo wa usimamizi wa faili nchini Brazil. Yaliundwa mnamo 2 Januari 1838 ina makao makuu yake huko Rio de Janeiro. Kwa mujibu wa sheria ya kumbukumbu ya Januari 8, 1991, ina wajibu wa kuandaa, kuhifadhi, kutoa na kufungua urithi wa nyaraka za serikali ya shirikisho, kutumikia Jimbo na wananchi. Mkusanyiko wa Masijala ya Taifa ina kilomita 55 ya nyaraka za maandishi; picha 2.240.000 na vigezo; vielelezo 27.000, katuni; ramani 75.000 na mipango; 7000 diski na kanda za sauti za magnetic 2000; Rolls 90.000 za filamu na kanda za video 12.000. Pia ina m ...

                                               

Misri (1805-1881)

Misri ni kipindi katika historia ya nchi ya Misri ambako mabadiliko mengi yalitokea yaliyopelekea jinsi Misri ya leo ilivyo. Mabadiliko haya yalikuwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kilikuwa ni kipindi cha mvuvuko wa nchi kutoka hali ya ukabaila kwenda katika uchumi wa kibepari. Ndani ya kipindi hiki Misri iliweza kujizatiti kutoka tawala za nje na hasa zile za Ulaya. Mifumo mbalimbali ya elimu ilianzishwa katika kipindi hiki. Pia mapinduzi ya nchi hii mnamo miaka ya 1881/1882 yalileta sura mpya katika nchi ya Misri hasa katika mtazamo wa dini ya kiislamu. Halikadhalika mapinduzi yalijari ...

                                               

Modibo Keïta

Modibo Keïta alikuwa Rais wa kwanza wa Mali na Waziri Mkuu wa Shirikisho la Mali. Aliongoza kwa kutumia itikadi ya Ujamaa wa Afrika.

                                               

Nasaba

Nasaba ikitumiwa kwenye masomo ya historia au siasa inataja ufuatano wa watawala hasa wafalme katika familia moja. Mtoto wa mfalme huwa mfalme tena na kadhalika. Neno laweza kutaja pia kipindi cha historia ambako familia fulani ilitawala. Kati ya nasaba za kifalme za leo ni hasa nasaba ya Matenno wa Japani iliyodumu muda mrefu. Tangu Tenno wa kwanza ni watawala 125 wanaohesabiwa katika familia hiyohiyo hadi Kaisari au Tenno Akihito wa leo. Nasaba nyingine inyojulikana duniani ni Windsor na malkia Elizabeth II wa Uingereza ni wa nne katika nasaba hii nchini Uingereza. Katika Afrika familia ...

                                               

Palantolojia

Palantolojia "kiumbe" na λόγος lògos "somo") ni fani ya sayansi inayochunguza masalio ya viumbehai katika miamba kama mwongozo wa historia ya uhai duniani.

                                               

Pango la Denisova

Pango la Denisova linapatikana katika milima ya Altai, Siberia, Urusi. Ni muhimu katika utafiti juu ya asili ya binadamu kutokana na upatikanaji wa mabaki ya aina mbalimbali za viumbehai wa jenasi Homo. Aina mojawapo imepewa jina la pango hilo Denisova hominin au Homo denisova, nyingine ni maarufu kama Homo neanderthaliensis, mbali ya Homo sapiens sapiens. Mabaki hayo yanaonekana kuthibitisha kwamba aina hizo zilizaliana.

                                               

Sergei Ivanovich Rudenko

Sergei Ivanovich Rudenko alikuwa Mrusi mwanaanthropolojia na mwanaakiolojia maarufu ambaye aligundua na kuchimba makaburi ya Scythian, Pazyryk huko Siberia. Rudenko alikuwa mfuasi wa "Shule ya Ufaransa ya Anthropolojia" ya Paulo Broca. Alishiriki katika Tume ya Ramani ya Kijiografia ya Kirusi IRGO iliyoanzishwa mwaka wa 1910.

                                               

Historia ya Kiswahili

Historia ya Kiswahili imeanza takriban miaka 1000 iliyopita kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki. Neno Swahili lina asili ya Kiarabu: Sahil ina maana ya pwani; sawahil ’’as-sawāhilī’’ السواحلي ni wingi wake kwa kumaanisha yote yanayohusiana na pwani, watu au utamaduni wa eneo la pwani. Katika Tanzania Kiswahili kimekuwa lugha rasmi ya serikali na taifa. Shule za msingi hutumia Kiswahili lakini shule za sekondari na vyuo bado zinaendelea kufundisha kwa Kiingereza. Tarehe 15 Februari 2015 rais Jakaya Kikwete alitangaza mpango wa kubadilisha lugha ya elimu nchini kwa kutumia Kiswahili kwenye n ...

                                               

Tarehe

Tarehe ni namna ya kutaja historia, lakini kwa kawaida zaidi nafasi ya siku fulani ndani ya mfumo wa kalenda. Kwa kawaida tarehe inarejelea kalenda ya Gregori. Lakini ilhali kuna kalenda mbalimbali inawezekana kutaja na tarehe tofauti kwa siku ileile kutegemeana na kalenda inayorejelewa.

                                               

Tarehe za maisha ya Yesu

Tarehe za maisha ya Yesu zinakadiriwa ili kuzidi kumfahamu Yesu kadiri ya historia. Hii ni kwa sababu Injili na vitabu vingine juu yake havitaji kwa kawaida tarehe wala mwaka wa matukio vinavyoyasimulia. Hata hivyo, vikitaja watu wanaojulikana na historia kwa njia nyingine kwa mfano Kaisari Augusto na Kaisari Tiberi, au mambo mengine ya namna hiyo, inaweza kujua kwa kiasi kikubwa au kidogo mwaka au hata tarehe ya matukio hayo. Muhimu zaidi ni kukadiria Yesu alizaliwa akafariki lini. Kuhusu kuzaliwa kwake, inajulikana kuwa kulitokea chini ya mfalme Herode Mkuu, aliyetawala hadi alipofariki ...

                                               

Ukomeshaji wa Biashara ya Watumwa

Ukomeshaji wa biashara ya watumwa ni mchakato au mlolongo wa matukio yaliyopelekea ufutaji au usitishaji wa biashara ya watumwa katika karne ya 19. Biashara ya watumwa ilikuwa biashara iliyodhalilisha utu wa binadamu, hasa Waafrika ambao ndio waliotumika kwa kiasi kikubwa katika biashara hiyo. Basi, baadhi ya watu Ulaya waliweza kuona madhara mbalimbali yaliyotokana na biashara hiyo hatarishi, na kuamua kuanzisha tapo la kuikomesha. Wengi wao walikuwa watu wa dini waliosukumwa na sababu za ubinadamu. Baadaye mataifa kama Uingereza yaliongeza bidii katika ukomeshaji wa biashara ya utumwa. K ...

                                               

Ustaarabu

Ustaarabu ni aina ya utamaduni uliyoendelea. Katika fani ya historia "ustaarabu" kwa Kiingereza civilization ni hali ya jamii iliyoendelea juu ya kuishi katika jumuiya ndogo zinazojitegema katika mahitaji yote. Kwenye hali ya ustaarabu watu wanashirikiana katika eneo kubwa zaidi, huwa na namna ya serikali. Shughuli zinagawanywa kati ya vikundi, matabaka na kazi mbalimbali chini ya kanuni na sheria zinazosimamiwa na mtawala au serikali. Katika historia ustaarabu kwa maana hii ulitokea penye kilimo ambako wakulima walianza kutoa sehemu ya mapato yao kwa mtawala au serikali fulani. Mapato hay ...

                                               

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka 1914 hadi 1918. Mataifa wapiganaji yalikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria, Bulgaria na Uturuki kwa upande mmoja dhidi ya Ufaransa, Urusi, Uingereza, Italia, Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo. Vita hii ilianza katika Ulaya ikapanuka haraka hadi Mashariki ya Kati, Afrika na Asia ya Mashariki ikasababisha kifo cha takriban watu milioni tisa.

                                               

Vita Kuu ya Pili ya Dunia

Infobox collage for WWII.PNG Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa vita iliyodumu kuanzia mwaka 1939 hadi 1945 kati ya Ujerumani, Italia, Japani na mataifa yaliyoshikamana nazo Romania, Hungaria na Bulgaria dhidi ya nchi nyingi za dunia ziliitwa mataifa ya ushirikiano kati yake hasa Uingereza, Uchina, Urusi na Marekani.

                                               

Waraka

Waraka ni hati yenye taarifa maalumu. Kwa kawaida, siku hizi waraka unaandikwa katika karatasi. Katika Biblia ya Kikristo mna nyaraka mbalimbali ambazo pamoja na barua zinafikia idadi ya 21, kwa mfano: Waraka kwa Waebrania. Katika utarakilishi, waraka pepe kwa Kiingereza: electronic document ni hati pepe inayotumika katika tarakalishi. Waraka pepe ni kama waraka wa kawaida ila data ni za elektroniki.

Historia ya Japani
                                               

Historia ya Japani

Historia ya Japani inahusu eneo ambalo leo linaunda ufalme wa Japani. Visiwa vyake vilikaliwa na binadamu tangu miaka 30.000 KK. Wakazi wa sasa wametokana na mchanganyiko wa makabila asili kama Waainu na Wakorea waliovamia visiwa hivyo kuanzia 500 KK.

                                               

Aathari

Aathari ni masalio ya vitu na utamaduni wa watu fulani. Mfano wa masalia ni magofu ya kale, vitu vya utamaduni na kadhalika. Wataalamu wa akiolojia ndio wanaotafuta na kuchunguza mabaki hayo ili kuelewa zaidi mambo ya kale yalikuwaje na watu wa wakati huo waliishi vipi.

Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →