Back

ⓘ Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga ni umoja wa kimataifa wa kampuni za usafiri kwa ndege. Makao makuu yake yako Montreal, Quebec nchini Kanada ambako kuna ..Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga
                                     

ⓘ Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga

Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga ni umoja wa kimataifa wa kampuni za usafiri kwa ndege. Makao makuu yake yako Montreal, Quebec nchini Kanada ambako kuna pia makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Kiraia.

IATA ilianzishwa mwaka 1945 ili kujenga ushirikiano wa makampuni makubwa ya ndege. Leo hii kuna takriban kampuni wanachama 240. Haya ni hasa makampuni ya kitaifa au makampuni makubwa ya kibiashara yanayotoa huduma za kimataifa. Mashirika madogo yanayohudumia nchi moja tu, pamoja na mashirika ya ndege za kukodi, mara nyingi si wanachama.

Kati ya kazi za IATA ni jitihada za kusanifisha tiketi za usafiri wa ndege kwa shabaha ya kuwezesha abiria kusafiri kwa mashirika mabalimbali kwa kutumia tiketi 1 tu. IATA inasaidia pia mapatano kati ya mashirika wanachama kukubaliana kati yao tiketi za makampuni mengine.

Kazi muhimu nyingine ni kutoa kodi fupi kwa kila shirika na kila uwanja wa ndege. IATA inalenga pia kusanifisha taratibu za usalama kati ya makampuni ya usafiri kwa ndege.

Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →